
SEHEMU YA 1 Basi siku hio shangazi yangu amenituma sokoni, na shangazi yangu ni mkali kama pilipili, yaan vipigo ana vyovipata kutoka kwa mume wake huwa anataka kunimalizia mimi kila siku, sijui hata nimeshawah kumkosea nini huyu shangazi mimi, ila hata siku moja sikuwah kubishana nae, kwa sababu kwanza sina pa kwenda, mama yangu alishafariki na baba yangu nae alishaoa zake muda mrefu na ndio maana akanipeleka nikakae na dada yake kwa sababu mke wake hakuwa ananitaka hata kidogo… Hapa kwa shangazi hakuna rangi ambayo sikuwah kuacha kuiona, Kama ni vipigo na matusi nilishavizoea sana, na matusi yakawa kama ndio
0 Comments