
Sijui ni kwanini maneno yake yaliniumiza sana, nilijua kuwa amefanya ya kufanya kwa sababu ananipenda sana, kumbe anajifanya kuwa alikuwa ananisaidia, sikuwa nataka kusaidiwa kabisa mimi, ila nilikuwa nataka anipende ili nikatambishie watu ambao walijua nitakuja kuteseka, na pia kwa sababu moyo wangu ulikuwa unamuhitaji sana…. “Kwanza sikukuomba unisaidie, nilikuwa nimeridhika kabisa kuolewa na Yule mzee, kwanza anamvuto sana, nina uhakika ningezaa vitoto vizuri sana, na kingine umesema kuwa umenisaidia kwa sababu unataman nije kuolewa na mwanaume ambae namtaka, basi mwanaume ninae mtaka ni mjeda sio wewe kwanza, anakaa huko mtaani kwetu, nikajibu kwa kujiamin, nikashangaa mwamba amenywea kama amemwagiwa
0 Comments