
Kwakweli sikuona Kama Ana umuhimu kwa wakati huo nilichofanya ni kumalizana na mapishi yangu na kwenda Kuwalisha watoto wangu. KWa Mara ya kwanza watoto wangu wakapata chakula wakiwa chumbani kwao lakini pia walikula bila baba Yao, Yaani niliamua kuishi maisha yangu tu, na nilikuwa tayali kuondoka pale kwa mume wangu Leo kesho Ila watoto wangu tu ndio waliniweka pale. Nikiwa nimetulia zangu chumbani kwangu, naperuzi tu mtandani gafla mlango wangu ulifunguliwa kwa nguvu sana na hamad ndio aliingia, Ila mapenzi yakiisha Walahi hakuna kitu unaweza kuogopa. Hamad aliingia chumbani kwangu akiwa amevimba kama mbogo lakini Wala sikushtuka Wala kuogopa zaidi
0 Comments