MY CRAZY HOUSE GIR 9---10

MY CRAZY HOUSE GIR 9---10

9 Weekend moja ilifika Damian siku hiyo alikuwa nyumbani hakwenda sehemu yoyote alikuwa akizunguka kwenye mazingira ya pale ndani. Kuna muda alikuwa bize kama anachati na mtu huku akitoa tabasamu . Vanessa alimuangalia na kutamani kwenda kumchukiza kidogo. Alisogea sehemu aliyokuwa ametulia na kusimama pembeni yake, Damiani alifunika simu yake na kumuuliza " Unataka nini? " Nimeliona unatabasamu ndio maana nikaja ..... " Khaaaaa kwahiyo tabasamu langu limekuvuta au? " Ningependa kujua unatabasamu kwaajili ya nini? " Wewe mwezi mchanga hebu ondoka hapa na ukafanya kazi zako. " Sawa kazi nitaenda kufanya lakini punguza ubinafsi nionyeshe hata kidogo na mimi

Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments