
Baada ya chakula cha usiku, Abby na Kamila walikaa sebuleni wajawa wanaangalia movies ya love story. Kamila alikuwa amelala mapajani kwa Abby akili ya kamila haikuwa kwenye movie alikuwa akimuangalia Abby “Baby... Kamila alimuita huku akishika kidevu cha Abby. “Naam, niambie mama” “Nahisi kama ndoto yangu imekuwa kweli. Mimi na wewe hapa… na hakuna mtu anaweza kututenganisha.” Abby alimtazama kwa macho ya upendo, kisha akashika kiganja chake kwa nguvu. “Naomba uamini maneno haya, Kamila… hakuna atakayeweza kututenganisha. Hata kama dunia nzima itasimama kinyume nasi, mimi na wewe tutapigana pamoja. Wakati wanaongea Rehema alikuwa anapita karibu yao na kusikia maneno yao.
0 Comments