
, mfanye ajisikie kuwa wa kipekee, furahika nae katika upendo ambao haujawahi kuonekana mahali popote, usiige upendo wa fulani, shindaneni kupendana vizuri pasipo kuumizana nafsi, itengenezeni dunia yenu ya upendo iwe yenye kuvutia na kupendeza kwenu wawili mlioamua kuishi ndani yake, hakuna kitu kitamu kama mapenzi ya wawili walioamua kuvuka vikwazo na kupendana kiukweli ukweli. tuanze hadithi yetu ya kuvutia sasa. ********* Gari ya la wagonjwa lilifika kwa kasi ndani ya hospitali ya taifa, kitanda cha wagonjwa kililetwa, mama aliwekwa juu ya kitanda hiko na kuanza kukimbizwa kupelekwa kwenye chumba maalumu cha matibabu, wakati wote uso wangu haukutamanika kwa machozi
0 Comments