
wako wamfanyie upasuaji..." Jasinta aliongea huku machozi yakimtiririka Mike ni Kijana mdogo tu, mbali na kumiliki pesa nyingi kajaliwa dharau. Alimuangalia Jasinta kwa kumkadiria, "Hebu mleteeni chakula kwanza...." Amri ilitolewa Chakula kiliwekwa mezani kisha Jasinta akaamriwa ale mpaka ashibe. "Tafadhali sana... naomba umsaidie binti yangu" Jasinta alizungumza huku akipambana kutafuna paja la kuku, kwa namna alivyokuwa anakula kwa kujiramba ni ngumu kuamini kama yupo hapa kusaidiwa. Sahani ya pili iliongezwa, Jasinta hakuvunga.... aliendelea kula huku akiomba msaada. "Huna haja ya kuomba sana....nitakusaidia endapo utakuwa tayari kufanya biashara na Mimi" Mike aliongea huku akikuna kichwa chake "Biashara ipi..." Jasinta aliuliza kwa
0 Comments