
"Unaelewa nini kuhusu neno Mtumwa "Sidhani kama kuna haja ya Mimi kukuelezea," "Nitakueleza kwa ufupi, Mtumwa ni mtu asiye na uhuru. Kama utakaa hapa hautakuwa na uhuru nata....." Kabla Ciara hajamaliza maneno yake Jessa alimkumbatia "Usimlaumu Mama katika hili, tamaa yangu ya kutaka kukuona ndio imefanya nije hapa" "Nakupenda mdogo wangu..... nitatafuta namna ya sisi kuwa Watumwa huru" Ciara aliongea Basi kwa pamoja walitoka nje, Katy akiwa juu ya kibaraza alimshuhudia Jessa. Moyo wake ulilipuka, tangu azaliwe hajawahi kuona msichana mrembo kama Jessa. Taratibu alishuka kwenye ngazi mpaka akawafikia "Naomba unifuate....." Katy alimuamrisha Jessa "Ni Mama yake Mike hutakiwi kumbishia
0 Comments