
Selim nilipokea na kuongea "hello babe " hakujibu akauliza "uko wapi ?'" Nilikaa kimya kwa sekunde maana nilihofia kwann asijibu salamu yangu ila kauliza niko wapi. Sasa nilivyo mjinga nikamdanganya kuwa niko kazin,akajibu poa na kukata sm nikampigia tena hakupokea nikamtumia meseji na kumuuliza "babe ni shida mbona kama hauko sawa" ujumbe ilifika ila hakujibu mh nikaona hapa kuna kitu . Sasa nika mpigia sim Nasra na kumuuliza kama walishatoka kazin akasema bado kwann nikajibu hapana napiga sm yake hapokei ,akawa amesema huenda akawa bz basi alivyonijibu vile nikatulia mda huo huo akingia Jacob . Tulisalimia na kukaa akaagiza kinywaji
0 Comments