
Baada ya Selim kutoka kwa hasira aliingia Nasra na mama mkwe wakawa wanauliza kimetokea nini , nilifuta machozi na kujibu hamna kitu ila ni mabishano kidogo tu . Walitoka na kuniacha mwenyewe nikabaki nikitafakari mambo yote toka siku aliyobadilika Selim , mawazo yangu yaliniambia huenda anatoka na Nasra ila moyo ulikataa kwani namuamini sana Selim . Nikahisi huenda ni hasira tu basi nikalala kesho yake asubuhi sikuwa na mood ya kwenda kazin ,nikaandaa chai na kumpigia Selim ila hakupokea nikachukua sm ya Nasra na kutuma meseji nikisema "hello uko salama " ilifika nikaka kusubiri kujibiwa . Hapo Nasra alikuwa chumbani
0 Comments