
Nililia pale chini akaniaga nakuondoka kwa maringo, nilimchukia Selim kuliko kawaida yani nikheri angeniacha kipindi kile kuliko kuja kuniacha saizi . Nilikaa pale nje kwa mda mrefu mpaka Jabir alivyorudi maana wakati ananifikisha nyumbani aliingia ndani na kutoka , alisimamisha gari na kuja kuniuliza shida nini mbona niko nje tena nalia . Sikumjibu nikampa talaka niliyokuwa nimeishika mkononi ,aliiangalia kawa kama hajaelewa na kuniuliza maswali lakin bado nilikaa kimya . Alivyoona siongei akainuka na kuingia ndani nikawa nasikia akigomba kwa ukali , hakuchukua mda akarudi nje na kutaka kunichukua ili aniriudishe ndani niligoma na kuinuka nikawa naondoka ila akanizuia sikutaka
0 Comments