
Simulizi za john 0789 824 178 1000 Nikasema, “Neema, ninaogopa! Siwezi kufanyiwa hivyo, tutakufa!” Neema akasema, “Sasa tutafanyaje? Tunakwepaje hapa?” Akasema, “Nawasikitikia wazazi wangu kwa kunileta huku.” Nikasema, “Unajua mbio, Neema? Unaweza kukimbia kwa kasi?” Neema akasema, “Ndiyo, naweza.” Nikasema, “Basi tukimbie!” Akasema, “Lakini tupo ndani ya msitu, tutaenda wapi?” Nikasema, “Ndiyo tukimbie, bora tukaliwe na wanyama kuliko ukatili huu. Mimi nakimbia, kama hutaki, baki, lakini sitaki kuwa kilema!” Neema akasema, “Tukimbie wote, hata mimi sibaki.” Tukahesabu, “Moja, mbili, tatu!” Tukaanza mbio kuelekea msituni ambapo tulikuwa tunaokota kuni. Sio sisi pekee, wasichana wengine watatu waliunga mkono, tukakimbia kwa kasi, mifuko
0 Comments