
Kwa majina naitwa Zawadi juma, mzaliwa wa Mkoani Pwani, Mtwara. Mama yangu alinizaa akiwa ameolewa na baba, lakini walitengana nilipokuwa darasa la nne. Baba alioa mwanamke mwingine na kuanza naye familia. Mama alipokuwa darasa la sita, naye akaolewa tena. Baada ya mama kuolewa, mumewe alisema hataki niishi nao, akidai kwamba ikiwa nitaishi nao, baba yangu mzazi na mama wataendelea kuwasiliana kwa kujifanya wananihusu. Hivyo, nikaenda kuishi na bibi yangu, mama wa mama, katika kijiji cha Mwagusi. Mama alikuwa anajitahidi sana kunihusisha, lakini hakuwa na kazi ya kudumu, alifanya biashara ndogo ndogo ambazo zilimudu tu pesa kidogo, ambazo hazikutosha mahitaji yangu
0 Comments