
Nilifanya uchunguzi wa zile karatasi nikagundua zile ni hisa za biashara kutoka kwenye makampuni mbalimbali na zile pesa niligundua kwamba sio pesa halali wala hazikuwa kwenye biashara, Lakini sakina alikuwa anaziingiza kwenye mfumo wa biashara ili zitumike kihalali, Inamaana hapo mimi nilikuwa nafanya kazi ya kutakatisha pesa bila mimi kujua. Nilipogundua mchezo ambao sakina anaucheza nilikaa kimya ili nione ni nani anayeuchezesha. Niliendelea kumpangia mipangilio mizuri ya pesa. Muda wa tina kuja kwangu ukawa umefika, Tina alinipigia simu na kuniambia nimpe maelezo ili achukuwe bodaboda aje hadi pale ninapofanyia kazi, Nikaona nikimruhusu tina aje pale ninapofanyia kazi, Sakina anaweza akafika
0 Comments