
Mh nilianza kujiuliza hadithi yake ina maana gani Lakini wakati natafakari, Gari la yule mzee lilikuwa tayari limesha kamilika kufanyiwa usafi, Yule mzee alinyanyuka na kuniambia usifikirie sana kuhusu jibu la swali langu lakini siku gari yangu imechafuka nitaileta kuja kuosha hapa sababu naona vijana wako wapo haraka sana. Yule mzee akawa ameondoka, lakini nilikuwa najiuliza kwani huyu mzee ni nani au ndio mume wa sakina, Sababu hadi wakati huo nilikuwa bado sielewi kama sakina ameolewa au hajaolewa, Badae nikapata muda wa kukutana na sakina, Nikamueleza kwamba kuna mzee alikuja kazini kwangu lakini sikumuelewa maana alianza kunisimulia hadithi za mafumbo,
0 Comments