
Ameelekea wapi nilianza kumtafuta maeneo yale lakini sikufanikiwa kumpata, Niliamua kwenda hadi nyumbani kwao na tina, Nilifika na kumkuta mama yake na tina anapika, Ilibidi nimdanganye kwamba tina nilimpatia vitabu vyangu anishikie lakini akaondoka navyo kama yupo huku nyumbani mwambie naomba anipatie, Mama yake na tina akaniambia, Tina bado hajafika nyumbani nahisi atakuwa amelala hukohuko bweni,sababu sio kawaida yake kufika nyumbani mida kama hii. Dah! Nilimwambia mama ahsante nitavichukuwa hata kesho huko shuleni. Nikawa nimeondoka lakini kichwa kinaniuma huyu tina yuko wapi, Nilianza kutapatapa kama nimechanganyikiwa, Nilirudi pale shuleni nikiwa kama mwendawazimu, Walinifuata wale marafiki zangu ambao tulitengeneza nao kengele,
0 Comments