
Tulipofika usawa ule ambao amesimama yule mwanamke, Yule mwanamke akatuita kaka zangu habari zenu, Tukamjibu poa, Akasema naombeni msaada wa mnisaidie kubadirisha spea tairi maana tairi moja limepata pancha. Tulitazamana mimi na marafiki zangu sababu hakuna hata mmoja kati yetu ambaye alishawahi kutengeneza gari wala kuziba pancha. Kisha rafiki yangu mmoja akasema sisi hatuwezi labda tukakuitie mafundi pale senta ili waje wabadirishe hilo tairi. Lakini mimi nikawaza kama niliweza kutengeneza kengele na watu wakaipenda hivi kweli nishindwe kubadirisha tairi la gari, Nikamwambia yule mwanamke hakuna shida tutabadirisha tairi sisi wenyewe, Yule rafiki yetu ambaye alisema hatuwezi yeye akakataa na kuondoka,
0 Comments