
Alikuwa ni yule mzee aliyekuja kazini kwangu na kuanza kunisimulia hadithi za mafumbo, Lakini pia vijana wake wale walioniteka walikuwa wameshika bunduki, Yule mzee alikaa kwenye kiti huku ameshika kitabu chake kilekile anachotembeaga nacho, Mzee akajitambulisha kwa jina la Nchima; Kisha akaniambia kijana naona leo umeamua kuja mwenyewe ili kuniletea majibu yangu,haya niambie kwenye ile hadithi yangu nani wa kulaumiwa? Nilimwambia mzee wangu usiniue nipo tayari nikuachie pale kazini kwangu ili uniache huru, Mzee alitoa kauli mpigeni. Wale vijana wake walioniteka walianza kunipiga na kunikanyaga kanyaga, Badae akawaambia acha (wakaacha) Kisha akaniuliza tena kwa mara ya pili swali ni lilelile,
0 Comments