
Nilimuuliza tina kwa nini inakuwa hivi, Tina alianza kulia kisha akatoa simu yake na kunionesha zile picha ambazo nilipiga na yule rafiki yake na sakina... (nilipoziona zile picha nikagundua kumbe ule ulikuwa ni mpango wa sakina ili aniweke mbali na tina) ... Nikajaribu kuongea na tina lakini alionekana kutokunielewa, Tina alianza kuongea huku analia... huna tena cha kunificha kama kunisaliti umenisaliti vya kutosha ulikuwa unanidanganya unafanya kazi ya kuosha magari kumbe una mapenzi ya siri na mwanamke ambaye amekuzidi hadi umri na anakutunza kwa kila kitu, sasa inatosha naomba uniache na maisha yangu kama kunitumia umenitumia sana, na kunichezea umenichezea
0 Comments