
Nikamwambia kwa sasa itakuwa ni vigumu lakini nitafikiria, Sakina akawa ameniomba sana siku hiyo ya mimi kutoa ushahidi nisikosekane, Lakini tina aliniangalia kwa kutamani kuongea na mimi ila sikujali nikaondoka zangu. Nilimpelekea Edina zawadi na alifurahi kweli lakini wakati huo zilibaki siku 20 ili kufunga ndoa mimi na Edina, Lakini pia nilikuwa bado sina simu nikawa nimefanya mpango nikanunua simu ila sikutaka Edina awe na simu sababu nilihofia akiwa na simu, Sakina anaweza akavuruga ndoa yetu isifanyike. Siku ya kwenda kutoa ushahidi ikawa imefika lakini niliwaza sana niende au nisiende, Nikaona bora niende ili nimalizane na Sakina, Tukaingia mahakamani kwa
0 Comments