
siwezi kukata vitunguu. Siyo kiburi ila sijui kupika... Mtoto wa kishua Mimi, wakati wengine wanafundishwa kushika njiti za kiberiti Mimi nilipatiwa mouse nicheze na kompyuta " "Mume wangu mtarajiwa jiandae kuhudhuria hotelini nadhani unajua Mimi ni mtu wa mishemishe sijui hata imeku...." Kabla hata Tasha hajamaliza maneno yake alidakwa kwa romance lililobeba hisia. Kila alipo furukuta ajitoe haikuwezekana, mwisho wa siku alitulia tuli. Basi Yolanda akiwa anakuja zake jikoni aangalie chakula kilicho salia alishtuka baada ya kuwafuma watu wakibadilishana mate. Bila kupoteza muda aliwapiga picha kisha akatupia mtandaoni. "Hatimaye Mrembo wa Tiktok kapata Mume atakaye saidiana naye kuosha vyombo "
0 Comments