
Salma alikaa kimya kwa sekunde kadhaa huku moyo wake ukidunda kwa kasi. Alijiuliza maswali mengi: "Nitamvutia kweli mama yake Fariss? Atanipokea kama mke wa mwanae? Je, akijua mimi ni mtoto wa uswahilini niliekuwa na maisha atanikubali kweli?" Alijiuliza maswali mengi sana lakini hakutaka kumuonyesha Fariss hofu hiyo. " Vipi mpenzi mbona upo kimnya? "Ni sawa mpenzi tutaenda. alisema kwa sauti ya chini. "Nitakuandalia kila kitu. Usijali, Fariss alimhakikishia hilo. " Sawa, naenda saluni basi kesho asubuhi utaniambia tunaenda muda gani. "Sawa. Nataka uvae kistaarabu, bila make up nyingi. Mama yangu ni mtu wa heshima sana, hapendi vitu vya kisasa kisasa
0 Comments