
Kijana Japhet alijikuta anaogopa sana baada ya kumuona kaka yake Lukasi yupo kwenye hali hiyo ya kukasirika. Baada ya Flora kumfikia Mume wake huyo akaweza kumkumbatia kwa furaha na kumpokea baadhi ya mizigo aliyokuja nayo. "Vipi Mume wangu mbona kama unaonekana haupo sawa, shida nini?" Flora alimuuliza Mume wake. "Hamna kitu Mke wangu mimi nipo sawa, ni uchovu tu wa safari nilionao" alisema Lukasi. Kijana Japhet naye akaweza kumsogelea kaka yake na kusalimiana naye halafu akampokea begi la mgongoni alilolibeba. Baada ya hapo wakaanza kuifuata ile gari ndogo aina ya Taxi sehemu ilipokuwa imepaki na baada ya kuifikia Taxi hiyo
0 Comments