
"Shemeji vipi tena mbona sikuelewi!?" Japhet aliuliza kwa mshangao. "Usihofu utanielewa tu taratibu" alisema Flora huku akiketi kitandani kwa Japhet. Japhet alibakia amesimama tu mle chumbani huku akimkodolea macho Shemeji yake Flora. "Vipi jamani mbona umesimama tu wima? hebu njoo basi Honey" alisema Flora kwa sauti ndogo ya kubembeleza. Japhet akashusha pumzi ndefu halafu akauliza: "Hivi Shemeji ni kwanini wewe unashindwa kujiheshimu?" Japhet aliuliza huku akiwa amekasirika. "Sio kama nashindwa kujiheshimu Japhet, tatizo ni wewe hapo unajitoa ufahamu" alisema Flora kwa kebehi. "Najitoa ufahamu kivipi?" Japhet aliuliza. "Usijifanye aujui Japhet, ina maana autambui kama mimi nakupenda?" Flora alisema huku akitabasamu.
0 Comments