
. Anaondoka nyumbani kwao na kuingia jiji Dar es salaam kwa dhumuni la kutafuta maisha, anajikuta akipata tabu kwa kukosa makazi ya kuishi jiji humo. Jua lake mvua yake, Elimu yake ya darasa la saba ikawa kikwazo kwake kupata kazi, hali iliyompelekea kujikita katika kazi ya kuomba omba barabarani. Maisha hayo yalikuwa endelevu kwa Walemi, lakini baadaye alibahatika kupata kazi nyingine ya kuuza chakula kwenye moja ya mgawahawa mitaa ya Mwananyamala.(Mama ntilie) Upole na ukarimu wa binti huyo anajikuta unampelekea kupendwa na kijana mtana shati, kijana msomi na mwenye pesa za kutosha, kijana nadhifu ambaye alimuona Walemi mara moja tu
0 Comments