
ILIPOISHIA....... Haikupita mda watu walianza kuja kila mtu alifika na kumpiga kibao na kukusanya fundo la mate mdomoni na kumtemea Yoashi........ ENDELEA NAYO... Watu wa kila aina walikuja na kufanya kama wenzao walivyokuwa wakifanya. Mashavu ya Yoashi yalivimba na alizimia kutokana na kupigwa makofi kwa mda mrefu huku mdomo wake ukitapakaa damu. Walinzi walifanya kama walivyopewa maagizo na Princess Herodia, walienda kumchukua Yoashi kwa ajili ya kwenda kumfungia. walimfikisha na kumpatia chakula ili aendelee kuishi wapate kumtese vizuri. Yoashi alikataa kula kitu kilichowakasilisha Walinzi, "Kula wewe mjinga" Mlinzi alimpa amri Yoashi na alikula bira kupenda huku chakula kikipita kwa tabu
0 Comments