
Sasha alijikuta anayalegeza macho kwa mshangao, pumzi ikimkatika kwa sekunde chache. Moyo wake ulikuwa unapiga kwa kasi, si kwa furaha, bali kwa hofu na mshangao mkubwa. Alimsukuma Issa kwa nguvu ndogo lakini yenye msimamo. “Hapana, Issa,” alisema kwa sauti iliyotikiswa na hasira iliyojificha, “hii si sawa. Nimekuheshimu kama kaka wa rafiki yangu.” Issa alisimama kimya kwa muda, macho yake yakibadilika ghafla. Alionekana kugundua kosa lake. “Samahani,” alisema kwa sauti ya chini, akirudisha mikono yake nyuma. “Nilizidisha mipaka. Sikupaswa kufanya hivyo.” Kimya kizito kikatawala sebuleni. Sasha alijisikia baridi moyoni. Hakutaka kubaki tena pale. Aliinuka haraka, akachukua mkoba wake. “Nadhani ni bora
0 Comments