
ENDELEA....... "Nimesema lala ni kukague au nikuitie nguvu kazi " Malkia Shamsa alifoka. Nguvu kazi tena jamani nilianguka chini kuomba msamaha. "Leo siyo siku ya kusamehe naomba uache kuongea neno nisamehe 😠" Malkia Shamsa alifoka huku akinirushia teke. Nilijitia kuumia kumtia moyo lakini ukweli kutoka moyoni sikuumia. "Malkia, kila kitu kimetokea kwa bahati mbaya, naomba unisamehe tafadhali, kama utaniua nitaweka wapi sura yangu " Niliomboleza. "Kesho asubuhi na mapema utaondoka hapa....kwa usiku mzima nitakesha nikifikiria kosa litakalo kufaa na hata hivyo na rahisisha mambo kwa sababu ya Baba yako. Kanifundisha sana mambo mengi kabla sijaja hapa hivyo nitakupunguzia adhabu "
0 Comments