
ENDELEA...... Safari ya kurudi Ikulu ilianza, ndani ya moyo wangu nilikuwa na mashaka. Sikuamini kama naenda kufanya kazi kweli, isije kuwa ni mbinu ya Mfalme kwenda kunichinja kwa kosa la kutia nguo ya Kijana wake kwenye furushi. Akili ya kuomba msamaha iliniijia, nilidondoka chini ni kapiga magoti katikati ya safari. "Sikuchukua nguo ya Kijana wako kwa ubaya....si unajua nimemlea yule. Basi hali ya kuwa naangalia nguo zake kila ni kimkumbuka ilinitawala " Niliongea. "Nakupeleka kule uwe Kijakazi wangu na si vinginevyo hayo makosa yaliyo kuondoa Ikulu Mimi hayanihusu" Mfalme Pangani aliongea. "Hayakuhusu na huku Malkia Shamsa ndio amenifukuza, huoni kama
0 Comments