
Linda aliamka asubuhi iliyofuata na kitu cha kwanza kumjia kichwani ni Alex. Alimtazama na bado alikuwa amelala fofofo. Alugusa shavu lake na kutabasamu kabla ya kumbusu . "Nakupenda Alex" alisema na kusimama haraka kisha akakimbilia bafuni. Alitoka dakika chache baadaye na sasa Alex yuko macho, akibonyeza simu yake. "Habari za asubuhi babe" alimsalimia na akatazama juu "Habari za asubuhi kipenzi akajibu Alex . Usiku ulikuwaje" Alex aliuliza na Linda katabasamu "Ulikuwa mzuri sijui kwako" akajibu Linda "Ulikuwa mbaya sana, niliota ndoto mbaya kwani haukunibusu usiku wa jana" alisema Alex na Linda akatabasam . “unapenda kunifanya nione haya kila wakati” akasema
0 Comments