BINAMU WEWE UNGEWEZA? SEHEMU 09

BINAMU WEWE UNGEWEZA?   SEHEMU 09

ENDELEA........ Nimepindua meza sasa na hakuna kitu mtaweza kunifanya" Baada ya kusema hayo wawili hao waliondoka. Mama na mdogo wangu walinifariji. Sikuwaelewa kwakweli kwa jinsi ninavyompenda Sony tena ndiye mwanaume wangu wa kwanza niliumia mno. Siku hiyo nililala nyumbani. Majira ya asubuhi niliamka nikajianda kwenda kazini kama kawaida. Nilifika kazini boss alipofika tu aliniita ofisini kwake. "Nice nisamehe najua nimekuumiza" Alianza kujiongelesha. "Hapa sio mahala pake boss" "Yaani unataka kunipangia cha kufanya au cha kuongea umesahau mimi ni nani kwako?" Sony aliongea kwa ukali "Lakini Sony kwanini unapenda kuniumiza eeeeeh! Kosa langu mimi ni nini mpaka umekuwa mwiba moyoni mwangu?"

Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments