
SEHEMU YA 06 "Baba, hapana! Tafadhali usimuumize!" Aisha alipiga kelele huku akijitupa mbele ya Ayman, akimkinga kwa mwili wake. Machozi yalikuwa yakimtiririka mfululizo, akishikilia nguo za baba yake. "Ayman hajanifanya kibaya chochote! Mimi ndiye niliyemfuata na kumpa chakula!" Mzee Salim alizidi kufura kwa hasira kuona binti yake wa pekee anajidhalilisha kwa ajili ya kijana wa makopo. "Aisha, unamkinga huyu mchafu? Una laana wewe?!" alifoka na kumvuta Aisha kwa nguvu, akimtupa nyuma ya walinzi. Walinzi wale wawili wenye miili mikubwa walimsogelea Ayman. Ayman alisimama kwa unyonge, akijua hana nguvu ya kupambana nao. Mlinzi mmoja alimpiga ngumi nzito ya tumbo iliyomfanya Ayman
0 Comments