
Muda ulionekana kusimama kwa sekunde hiyo moja. Macho ya Ayman yalishuhudia kifo kikitapika giza mbele yake. Alijaribu kuruka upande wa pili ili kujiokoa, lakini miguu yake iliyokuwa imechoka na kuishiwa nguvu kutokana na njaa haikutii amri ya ubongo wake. PAAAAH! Kishindo kikubwa na cha kutisha kilipasua upweke wa usiku ule wa mvua. Lori lile lilimgonga Ayman kwa nguvu kubwa upande wa mbavu zake za kulia, likamnyanyua juu angani umbali wa mita kadhaa, na kumtupa kwa kishindo kikubwa chini kwenye kingo za mawe zilizochongwa za mtaro mkubwa wa Buguruni. Kichwa chake kiligonga kingo ya jiwe, na damu nzito nyekundu ilianza kububujika
0 Comments