
“Una maanisha nini? Ikabidi na mimi niulize… “Mimi ndio niliekuoa, akasema .. Nikatoa macho, kisha nikamuuliza “Kwani unaitwa nani… “Naitwa Erick Resmund na nadhani ndio jina ulilolisikia wakati nakuoa, au ulisikia jina lingine tofauti?.. “Kumbe wewe ndio Erick , sasa kwanini haukunambia wakati wote huo mpaka nikajua umeniteka, nikazidi kuongea, akatabasamu kisha akanambia “Yaan akili yako ni ndogo sana, ndio nimekuteka ila haujawah hata mara moja kujiuliza kwanini ulivyofika nyumban kwangu ulikuwa kaparty kidogo, ujue kuwa nilikuwa nimejipanga ila si unajua mm ni muhuni, nilitaka kumchukua mke wangu kwa namna ya tofauti tu, akasema … “Sasa Yule mzee ni nani?
0 Comments