
Mama yake ni kama hakuwa anataka kumuelewa, ila nikamsikia baba yake anampooza mkewe, nikarudi zangu chumban kwangu nisije nikakutwa bure… Nikajikuta naanza kuwa na hofu sana, kwanza nikafunga mlango vizuri sana siku hio, niliogopa nisije nikanyongewa ndani bure, au nikatupiwa masumu, nilikuwa naogopa mno, na siku hio sikutoka ndani kabisa, nikaamka mapema sana, nikafanya kazi zangu haraka haraka, mara mama akatoka, nikamsalimia hata hakuitika, nikajua ehee kasheshe imeanza, ila nilipomsalimia baba akatabasamu na kuniomba nimpikie chai… Nikapika haraka haraka, kisha nikamtengea, wakati huo mama alikuwa ameondoka, na omari alikuwa bado chumban kwake.. “ mwanangu mzoee mama yako kuna muda anakuwa
0 Comments