
Safari yangu iliishia kwenye glossary moja hivi ya hapa.mtaani kwetu...hivi niliwaambia ni wapi naishi?naishi manzese sio mbali sana ila ni hapo naishi....manzese shimoni huko ndo kwetu....kama mjuavyo maeneo ya huko..hakuja poa hata kidogo..pale nilipokaa tu kwenye glossary hawakuacha kunifata wale wadau wangu na kununua bia ...hawakuacha kuniagizia gongo pia..ndio kinywaji changu pambe nikielewacho😁. "Huwenda si mwanamke wewe haiwezekani"nilisikia sauti ngeni ya kiume ikiniongelesha. "Ni heri ukakaa kimya kujiepusha na vurunguti langu kuliko kuingilia mtu usiyenijua kabisa ni wazi unapenda matatizo ya kujitakia wewe mtu"nilizungumza. "Ni ajabu hii hakika"sauti za washkaji zangu zilisikika zikizungumza pale baada ya yule mkaka kunisogelea karibu
0 Comments