
MR. AB Tulipoishia Ile nimefika sebuleni kulikuwa na giza, nikapapasa swichi na kuwasha taa. Sikuamini, nimewasha taa hivi, naona mwanaume kasimama katikati ya chumba amevaa boxer tu, ana tattoo zake ameinamisha kichwa chini. Kuinua uso hivi sio mwingine ni yule mwanaume ambaye ametoka kwangu mchana, ambaye alijiita Jerry kama jina la mume wangu. Kidogo nizimie. Endelea “Shindwa pepo” Nilisema kwa sauti kubwa huku moyo ukienda kasi “Haha......” Nilishangaa yule kijana amecheka huku akinitazama kwa furaha, alionekana kutokuwa na lengo la kunidhuru. “Yesu nisaidie” Nilijisemea kimoyo moyo huku nikisogea nyuma ili nikimbilie ndani. Hakufanya chochote alizidi kusimama pale sebuleni ni nikaingia
0 Comments