
DOLLAR: ( DAKTARI WA HUBA ) Sehemu ya Pili Mtunzi: Layman Donsue Siku iliyoanza kama kawaida chuoni iligeuka kuwa sinema ya bure. Mvulana yule aliyeuliza swali gumu kwa Dollar "Wewe mwenyewe unajua kupenda au ni maneno tu?" hakuwa mtoto wa kawaida. Alikuwa na jina la ajabu sana. Aliitwa Mtangazaji, lakini hakuwa na kipindi chochote. Alijieleza kuwa ni mtangazaji wa hisia, mawazo na mitetemo ya moyo. Mtangazaji hakuvaa kama mwanafunzi wa kawaida. Wakati wengine walivaa jeans na T-shirt, yeye alivaa kaunda suti ya pinki na tai ya njano. Viatu vyake vilikuwa vinalia kila akitembea kama mtu aliyekanyaga mbata wa plastiki. Alipotokea
0 Comments