
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia Lucas Zacharia Kanyenze (64) mkulima na mkazi wa Hyamvisi Wilayani Ruhembe Mkoani humo kwa tuhuma za mauaji ya Kasimu Said Kandulu (52) mkulima mkazi wa Simbalambende kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali kifuani upande wa kushoto. Taarifa ya leo Mei 30, 2025 iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro SACP. Alex Mkama imeeleza kuwa tukio hilo limetokea Mei 26, 2025 katika kijiji cha Simbalambende kata ya Ruaha wilaya ya kipolisi Ruhembe ambapo Kandulu amepoteza maisha huku chanzo cha tukio hilo likitajwa kuwa ni wivu wa kimapenzi ambapo marehemu alikuwa anamtuhumu mtuhumiwa kwa
0 Comments