
MIMBA YA BESTMAN 7 Mulky alikuwa kajiinamia anaangalia chini , Yasini alimshika begani huku akimuita jina lake. " Mulky.... Mulky alinyanyua kichwa akamuangalia " Mulky mke wangu hakuna mtu yoyote wa kuingilia maisha yetu naomba upuuzie kile ulicho tokea . " Nawezaje kupuuzia wakati kilichoongelewa kina ukweli ? Familia yako inatamani kuona unaitwa baba wanatamani kuona watoto waliruka ruka ndani ya hili jumba hata mama yako nahisi anatamani sana ila hajawa na ujasiri wa kuniambia. " Hata kama hawawezi kuingilia maisha yetu. Na kuhusu mama yangu hana Uswahili huo anaamini Mungu ndio mpangaji na mtoaji kwa yule ambae amepanga kumpa
0 Comments