
MTI UNAOMWAGIKA DAMU SEHEMU 1 Jua liliendelea kuangaza taratibu huku kiza kikizidi kuaga. Sauti za ndege zilisikika na kufanya asubuhi ile iwe yenye kuvutia. Wanawake walitoka ndani wakiwa na mafyagio, wengine vyombo vinavyotaliwa kuoshwa, wengine ndoo za maji kama walivyokuwa wakifanya siku zote asubuhi. Lakini asubuhi hiyo ilikuwa tofauti na siku zote. Waliokuwa wakienda visimani walikutana na maajabu yaliotisha. Si rahisi kustahimili hasa kwa wanawake. Hofu zikawatanda na wenye roho nyepesi walitimua mbio. Ilikuwa damu inayotiririka kutoka kwenye mti wa mbuyu ulio kando kidogo na makazi ya watu, njia ya kuelekea sokoni, visimani na hata wale wanaokwenda mashambani. "Hii siyo
0 Comments