
wakati nikiwa mdogo. Nilianza maisha ya kuhangaika tangu nikiwa mdogo baada ya wazazi wangu hao kufariki dunia. Nilianza kuajiriwa kazi ndogondogo ili nipate pesa za kujikimu na nilipofikia umri wa miaka kumi na minane ndipo nilipopata ajira rasmi. Ajira yenyewe ni ya kazi ya ulinzi. Niliajiriwa katika kampuni moja ya ulinzi, kazi yangu ikiwa ni kulinda zamu usiku. Kwa vile sikuwahi hata kupitia mafunzo ya mgambo nilifundishwa hapo hapo jinsi ya kutumia bunduki na jinsi ya kukabiliana na wezi na majambazi. Lindo langu la kwanza lilikuwa katika eneo la Gofu. Unapoingia katika jiji la Tanga eneo hilo unakutana nalo mwanzo
0 Comments