
Tulielekea kula, tulipofika kula mke wangu sasa anapiga picha kila kitu, mara nipige picha. Mimi tena ndiyo mpiga picha, chakula kinapigwa picha mpaka nachukia na ni muda wa kula. Alipomaliza alitabasamu na kusema “tule sasa Hubby.” Nilishusha pumzi tu, alichukua uma wangu na kunilisha. Kisha aliendelea kula huku akiwa anazungumzia ndoa yetu namna imeenda viral, watu wanazungumzia, marafiki zake na zawadi. Mimi nilikuwa nakula, namuwaza yule binti niliyemuona kanisani. Kisha nilikuwa nashindwa kabisa kujizuia kutabasamu. Nilijikuta natabasamu tena tabasamu pana kabisa. Mke wangu alinitazama na kuniita kwa Jina langu “Ricky!!” Mimi nikaendelea tabasamu, akaniita tena “Ricky!!” Nilimtazama na kusema “Naam!!”
0 Comments