
Tunapanga vitu huku yeye na simu, akimaliza anaweka pembeni kidogo inaita mpaka nachukia sasa niliamua nijikaze kama alivyosema wapo kwenye matatizo. Dereva alipiga simu kuwa amefika, nilimuelekeza afuate mizigo na kisha tuendelee na safari. Unajua tangu tunaingia ndani ya gari, mpaka tunafika nyumbani mke wangu na simu tu. Sikupenda kabisa hii tabia. Lakini nitafanyaje na nimeambiwa tayari kuwa ana matatizo. Nilishuka na mke wangu, kama ambavyo ipo nyumba ni mpya lakini kila kitu kipo vizuri kabisa. Madam ambaye tumeandaliwa pale nyumbani alitupokea. Niliingia ndani na mke wangu. Hakuoga hata zaidi alibadilisha nguo tu, alinibusu huku anaongea na simu na kuondoka
0 Comments