
165 Tulicheka pamoja huku tunalia sana mpaka simu ikakata. Joan aliniinua pale chini na kunikumbatia. Alinikumbatia na kuniambia “uliniambia nisilie nimumini Mungu, niombe kwa nguvu, ulinifuta machozi Ndeana. Sitaki kuamini wewe ni mdhaifu namna hii. Kwasasa wewe unatakiwa sana kusimama kidete kutetea penzi lako. Kuwa makini sana, muombe Mungu na msaidie mwenzako. Sikia Stewart ni Tajiri, ana watu wenye pesa. Anajua apite wapi na wapi apite kufikia malengo. Anaumia kwasababu kapoteza ila hawezi poteza milele. Na hata hivyo pengine tayari ana mipango anataka tu wewe ndiyo upambane kufikia ndoto zake yaani umsaidie kwa mawazo, umpe utulivu na vitu kama hivyo.
0 Comments