
Namna ambavyo alikuwa anatembea, niliogopa sana. Alikuwa anaonekana amekasirika. Hata ofisini hatukufika kwakweli, alinivuta kwenye moja ya kona ambazo zipo ndani ya ile hotel. Kisha alinitazama usoni. Macho yake tayari yamebadilika. Nilikuwa nataka nimuulize kuna nini, ila aliniwahi yeye ndiye aliyeniuliza kwa sauti yenye maumivu aliuliza “Alikuwa anasemaje?” Nikamtazama na kumuuliza “Nani tena?” Akaniambia “acha kunidanganya, nimeona kila kitu akakupa na kadi yake. Niambie alikuwa anataka nini?” Nikajikuta nimecheka. Yeye hata hakucheka badala yake akasema “unaona sasa unanicheka, unaniona mimi mpumbavu sina akili. Ndeana acha masihara mimi naumia roho.” Akaniachia na kwenda kuegemeza kichwa ukutani hivi. Nilicheka kidogo ndani yangu.
0 Comments