
. "Sikuwahi kufanya kitu kama hicho, kwanini unanifanyia hivi jamani? Ni Joel alinitongoza yeye mwenyewe na nilimkatalia." Mia alianza kulia. "Usiniletee uchuro hapo nje, kama unataka kulia nenda huko sio hapa. Na kama kipaji chako ni kulia basi nenda kalie misibani watakulipa." Mira aliongea akiwa ndani. Wapangaji wengine walimuonea huruma Mia. "Mia njoo huku." Shufaa alimshika mkono Mia akaingia naye kwake chumba chake. "Acha kulia basi, unajua utapata homa bure." Shufaa alijitahidi kumbembeleza Mia. "Naumia sana Shufaa, sikuwahi kutetemeka. Dada yangu atanichukulia mimi kama takataka." Mia alizidisha kulla. "Acha basi kulia shoga yangu, achana naye. Huenda kuna mambo ya kazini
0 Comments