
kucheza nao..." Mira alimkatisha Gael. "Kwahiyo hii ndo sehemu nzuri uliyoniambia?" "Ndiyo sweetie, hapa kuna furaha ya kweli. Twende ndani, ukajionee mwenyewe." Gael alimfungulia Mira mlango, akashuka. Waliingia kwenye geti dogo. "Gael, mbona umechelewa sana leo?" Mr. Maximilian alimuuliza Gael. "Nilikuwa na kazi nyingi sana baba, lakini kwa bahati nimewahi kidogo kufika." "Na huyu amefuata nini hapa?" Bi Helen alimuuliza Gael. "Mama, huyu ni mpenzi wangu. Ana haki ya kuwa hapa, na nina haki ya kwenda naye popote ninapotaka, alijibu Gael bila uoga huku ameushika mkono wa Mira. "Unamjibu vipi hivyo mama yako!" Mr. Maximilian alikasirika sana. "Mume wangu, acha
0 Comments