
tafadhali, Gael aliongea kwa sauti ya upole Mia alimuonea huruma Gael. "Sawa nitabaki lakini niahidi kesho mapema sana tutaenda hospital." "Nakuahidi kesho nitaenda hospital," Gael alijibu huku anatabasamu. Mia alimsaidia Gael kusimama wakaenda kukaa kwenye kochi. "Mbona unaniangalia hivyo?" Mia alimuuliza Gael "Kwa sababu wewe ni mwanamke wa tofauti sana na wanawake wote niliowahi kuwa nao karibu, atakae kuoa atakuwa na bahati sana... natamani hiyo bahati ingeniangukia mimi," Gael alipitisha mkono wake kwenye shingo ya Mia. Mia aliutoa mkono wa Gael akasogea pembeni. "Acha utani wako bhana Gael wewe si una mpenzi... unatakiwa kupumzika kesho uende hospital," Mia alitaka kusimama,
0 Comments