
*CHAGUO SAHIHI* SEHEMU YA....3 Na Mamuh Mohd (0716730000) Tulipoishia...... Manga alijibu kwa kutikisa kichwa na basi akarudi kuendeleza na majukumu yake..... SONGA NAYO...... Bi.mwamvua na binti yake mambo yaliwageukia ilibidi sasa wakapange nguo zao waondoke. Hawakutegemea kama Jarden angewatolea uvivu wa namna ile. "Mama tungemuomba msamaha tukabaki kuendelea kukaa hapa mama". "Mwanangu tumefeli wewe huoni kwa jinsi alivyoongea anaonekana kabisa anatuchukia, hatuwezi tena kukaa hapa mwanangu elewa hilo". Basi walijiandaa na siku iliyofuata asubuhi na mapema waliondoka zao. ******** Baada ya siku mbili kupita mrembo wa kuitwa Nancy alianza kazi katika ofisi ya Mr jarden baada ya kufuzu katika Usahili
0 Comments